9 Agosti 2021 - 11:20
Kuendelea ukiukaji wa haki za binadamu Bahrain katika kivuli cha kimya angamizi cha kimataifa

Miaka 10 imepita tokea kuanza harakati za mapinduzi ya watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa, harakati ambazo zilizimwa kwa muda na kwa mkono wa chuma wa msaada wa kijeshi wa utawala mwingine kandamizi wa Aal Saud nchini Saudia, msaada ambao hatimaye umepelekea watu wa nchi hiyo kukandamizwa, kuteswa na kuuawa kinyama.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Licha ya ukandamizaji huo ambao umeendelea kwa miaka kumi sasa, ukiwemo wa vifungo vya miaka mingi jela na kuuawa vijana wa kimapinduzi wa Bahrain, lakini watu wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi wangali wanaendelea kupigania haki zao za msingi za kufanyika mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini. Katika uwanja huo Ijumaa wakazi wa mtaa wa Sanabis walifanya maandamano ya amani wakisisitiza juu ya udharura wa kuachiliwa bila masharti wafungwa wote wa kisiasa wa nchi hiyo, na kuongeza kuwa hawatalegesa msimamo wao kuhusiana na jambo hilo. Walibeba picha za baadhi ya wafungwa katika maandamano hayo na kutaka wote waachiliwe mara moja.

Maandamano ya watu wa Bahrain yamekuwa yakiendelea katika hali ambayo utawala wa Aal Khalifa umekuwa ukitumia kila mbinu ya kidikteta kuyakandamiza huku taasisi na mashirika ya kimataifa yanayodai kutetea haki za binadamu yakiwa yamekaa kimya mbele ya unyama na ukanadamizaji unaofanywa na utawala huo dhidi ya raia wake. Iwapo yamechuku hatua yoyote basi imekuwa ni ya kutoa taarifa na kulaani jambo hilo kwa maneno matupu yasiyo na uzito wowote wa wahusika kufuatiliwa kisheria.

Kwa mfano Jumamosi iliyopita, Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International, lilitoa taarifa likitaka Hassan Mushaima' ambaye lilimtaja kuwa mmoja wa wafungwa mashuhuri zaidi wa kisiasa duniani, aachiliwe huru mara moja. Licha ya kutolewa misimamo kama hiyo lakini ni wazi kuwa utawala wa Aal Khalifa hauipi umuhimu wowote kutoka na uungaji mkono mkubwa unaopata kutoka kwa nchi za Magharibi na utawala haramu wa Israel. Kwa msingi huo unaendelea kukiuka na kukanyaga wazi wazi haki za kimsingi za raia wake bila kujali lolote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kabla ya hapo baadhi ya wabunge wa nchi za Ulaya walizitaka serikali zao ziwashinikize watawala wa Bahrain ili waheshimu haki za binadamu za watu wa nchi hiyo lakini hakuna lolote lililobadilika katika uwanja huo hadi sasa, bali watawala hao wamezidisha mateso na ukandamizaji wao dhidi ya wapinzani na wanaharakati wa nchi hiyo ndogo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.

Mwezi uliopita, Ali Mushaima' mwanaharakati ambaye pia ni mwanae Hassan Mushaima' Katibu Mkuu wa Harakati ya Haki ya nchini Bahrain alielezea wasiwasi mkubwa ilionao familia yake kuhusiana na kuendelea kuzorota kiafya hali ya baba yao huyo anayeshikiliwa kidhulma katika jela za utawala wa Aal Khalifa. Miaka mitatu iliyopita pia Shirika la Msamaha Duniani lilitoa ripoti likisema kuwa kufikia sasa Mushaima' amekuwa kifungoni kwa siku 3,730, bila kuhesabu vifungo alivyowahi kuhudumia huko nyuma.

Katika ripoti hiyo, shirika hilo lilisema kwamba hali mbaya ya haki za binadamu nchini Bahrain imewatia wasi wasi mkubwa wataalamu na wanaharakati wengi wa kimataifa wa kuteteta haki za binadamu. Kabla ya hapo mashinikizo na juhudi za kimataifa zilipelekea kuachiliwa huru wafungwa kadhaa wa kisiasa nhini Bahrain akiwemo Nabil Rajab na Najah Yusuf lakini Hassan Mushaima mwenye umri wa miaka 73 akaachwa nyuma na kuendelea kuhudumia kifungo cha dhulma kwenye jela za Aal Saud.

Utawala wa Aal Khalifa umaendelea kutesa na kuwakandamiza wafungwa wa kisiasa na kuwanyima haki zao za msingi katika hali ambayo mwaka ujao umepanga kufanya uchaguzi wa kimaonyesho kwa kutekeleza hatua kadhaa za kimaonyesho na vile vile kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

Kwa msingi huo taasisi na mashirika ya kimataifa yanapasa kuupa uzito maalumu ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na watawala wa kidikteta wa nchi kama Bahrain na Saudi Arabia dhidi ya raia wao, udikteta ambao unaendelea kufanywa katika kivuli cha kimya kikuu cha jamii ya kimataifa, badala ya kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya mataifa mengine huru na yanayojitawala.

342/